Uwanja wa uhuru ambao ulikuwa kwenye marekebisho chini ya wakandarasi umekamilika na Waziri Nape Nnauye amekabidhiwa.
Uwanja huo maarufu kama Shamba la bibi ulikuwa ukifanyiwa marekibisho na na kampuni Beijing Construction Engineering Group (BCEG).
Waziri Nape alisema kuwa kwa sasa ni jukumu la watanzania wote kuhakikisha wautunza uwanja huo kwa manufaa ya watanzania wote.
"Tunatakiwa kutunza na kulinda uwanja wetu kwa ajili ya manufaa ya watanzania, hii ni kwa ajili ya watanzania wote."Alisema Nape
Comments
Post a Comment