Kama ulikuwa hufahamu idadi ya wachezaji waliosajiliwa Simba basi bila shaka wachezaji hao watatambulishwa rasmi leo katika uwanja wa Taifa.
Leo ni maadhimisho ya Simba day katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam, ambapo wachezaji wapya wote waliosajiliwa Simba watatambulishwa rasmi.
Simba kupitia idara yake ya habari iliweka wazi kuwa mbali na utambulisho wa wachezaji pia timu hiyo itazindua uzi wake mpya utakao tumika kwenye ligi 2016/17.
Katika hafla hiyo bendi maarufu ya utumbuizaji Tanzania, twanga pepeta itaongoza shangwe na shamra shamra za sherehe hiyo.
Hata hivyo tukio la mwisho ni mechi ya kirafiki kati ya Simba na FC Leopard kutoka nchini Kenya ambapo Simba imewataka mashabiki wake kushuhudia makali ya kikosi hicho.

Comments
Post a Comment