Wazo la Azam FC, kutumia uwanja wake dhidi ya Simba na Yanga


Uongozi wa Azam unafikiria kuweka mpango wa kutumia uwanja wake wa nyumbani dhidi ya mechi ya Simba au Yanga.

Azam haioni sababu kwa nini timu ya Simba au Yanga zisikaribishwe kwenye uwanja wao nyumbani kama zinavyowasili timu zingine za ligi kuu.

Huenda muda wowote kuanzia uongozi huo ukashughurikia mpango huo TFF ili Azam iwe kuwa huru kutumia uwanja wake wa nyumbani baina ya timu hizo.

Licha ya Ukongwe na ukubwa wa baadhi ya timu duniani na wingi wa mashabiki wake wanalazimika na kuwajibika kucheza katika viwanja vya timu zisizo na majina ingawa huingiza idadi ndogo y mashabiki.

Mfano mzuri ni huwa ile michuano ya kombe la ligi England, hivyo Azam haioni sababu kwanini Simba na Yanga zisicheze na timu hiyo kwenye uwanja wake wa nyumbani licha ya kupokea kiwango kidogo cha mashabiki tofauti na uwanja wa taifa.

Nadhani TFF iangalie suala hili kwa umakini, ipo haja na haki ya kwa Azam FC kutumia uwanja wake wa nyumbani dhidi ya Simba na Yanga.

Comments