Wenger ahofia kustaafu


Arsene Wenge ambaye ni kocha wa Arsenal amesema kuwa anahofia siku ya yake ya kustaafu kuliko wakati wowote kwenye maisha yake.

Wenger alisema anahisi kutawaliwa na hofu siku atakayofikia maamuzi hayo, kwa kuwa ni ngumu kuacha kuishi katika maisha uliozoea.

"Ni ngumu sana kuachana na mpira moyoni mwangu nimejawa na hofu endapo nitachukua uamuzi wa kuachana na soka." Alisema Wenger

"Nakumbuka Sir Alex Ferguson alipostaafu soka aliinita tuweze kunywa pamoja mvinyo, nilimuuliza endapo moyo wake upo tayari kwa hilo, alinijibu hana uhakika." Aliongeza kocha huyo wa Arsenal

Wenger 66, anajiandaa kutimiza na kusherekea kipindi cha miaka 20 tangu alipotua october akitokea hiyo ilikuwa mwaka 1996.

Comments