Wenger ajiandaa kufanya matumizi


Kocha wa timu ya Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa timu hiyo ipo tayari kufanya usajili lakini kwa mpango maalum.

Hivi karibuni Wenger alishindwa kukamilisha usajili wa beki wa Valencia Shkodran Mustafi baada ya kukataa dau lililowekwa na Valencia.

Wenger aliongeza kuwa wapo nyota wengi wanasajiliwa England na kudhoofisha ligi hiyo kutokana na kulipwa mishahara mikubwa isiyoendana ubora wao na hivyo huzigharimu timu hizo wanapotolewa kwa mikopo.

"Tupo tayari kutumia kiasi kikubwa sokoni, lakini kwa wachezaji wanaostahili na pia kwa utaratibu maalum alisema Wenger." Alisema Wenger

Comments