Wenger: hatukuwa tayari


Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kuwa wachezaji hawakuwa tayari kimwili hali iliyopelekea kufungwa na Liverpool.

Arsenal ilifungwa mabao 4-3 na Liverpool ambapo Wenger ana imani kutokuwa fiti kwa baadhi ya wachezaji akiwemo Ramsey anayesumbuliwa na hamstring kumewapelekea wao kufanya vibaya.

Mechi hiyo pia haikuwahusisha Mesut Ozil na Oliver Giroud ambao bado wapo kwenye mapumziko baada ya kuzitumikia timu zao kwenye fainali za UEFA Euro mwezi uliopita.

"Wachezaji wangu bado hawana utayari kimwili, Ramsey ni mfano mzuri alipatwa na majeraha hakuweza kumaliza mechi, vile vile hatukuwa na Ozil pamoja na Giroud." Alisema Wenger

Comments