Timu ya West Ham maarufu kama wagonga nyundo leo imeaga rasmi michuano ya Europa ligi baada ya kufungwa bao moja 1-0 Astra Giurgiu.
West Ham ilishindwa kutamba katika uwanja mpya wa Olympic baada ya kuruhusu bao kipindi cha kwanza ambalo lilifungwa na Teixeira dakika ya 45.
Wiki iliyopita West Ham ilipata sare ya bao 1-1 ikiwa ugenini hivyo matokeo halisi ni 2-1 ambayo yameindoa rasmi timu hiyo kwenye michuano ya Europa.

Comments
Post a Comment