Yanga na matatizo ya penati baada ya dakika 90


Kama kawaida Yanga inaendelea na matatizo yake yale yale ikiwemo kukosa umakini katika penati baada ya dakika 90.

Hii ni mara ya pili naandika jambo hili, wakati Yanga ikifuzu kuingia hatua ya makundi kwenye kombe la shirikisho barani Afrika, nilitamani akazie jambo hili kwa kuwa ni muhimu kwenye mashindano.

Azam iliwapa Yanga wakati mgumu baada ya kuchomoa bao zote, anayeifahamu Yanga kuelekea penati kulishajenga hofu mioyoni mwao, sababu iko wazi hawafanyi vizuri katika hatua hii.

Niliandika makala fupi, nikisisitiza Pluijm anatakiwa kuandaa wakina Yondani watano, kwa wakati ule Kevin Yondani alikuwa mpigaji penati mzuri kwangu.

Yanga ni wazuri kupata matokeo ndani ya dakika 90, Azam ilipochomoa bao zote mbili na kuyafanya matokeo kuwa 2-2 tayari walishapata ushindi kwa asilimia 80.

Hakuna cha ajabu kama Azam waliichapa Yanga kwa mikwaju ya Penati 4-1, si jambo la kufikirika lakini nadhani Yanga hupata kitete kwenye hatua ya matuta. Yanga ni timu nzuri sana lakini na matuta ni muhimu pia.

Comments