Timu ya Yanga imerejesha matumaini huenda ikavuka kuelekea nusu fainali baada ya kuifunga MO Bejaia bao 1-0.
Kwa matokeo hayo yanaifanya yanga kukusanya idadi ya pointi 4 nyuma ya MO Bejaia na Medeama ya Ghana ambayo itashuka dimbani dhidi ya TP Mazembe kesho.
Endapo Medeama itapata ushindi ya TP Mazembe Yanga atakwenda kukamilisha ratiba Lubumbashi katika mechi ya mwisho dhidi ya Mazembe.
Kushinda kwa TP Mazembe kesho kutainua zaidi safari ya matumaini kwa Yanga ambao wanatakiwa kufanya kazi ya ziada kumfunga TP Mazembe nyumbani.

Comments
Post a Comment