Beki kisiki wa Yanga Kelvin Yondani atakaosa mechi ya TP Mazembe, jijini Lubumbashi Agosti 23 mwaka huu kutokana na kadi mbili za njano.
Yondani anampokea Donald Ngoma ambaye alikosa mechi dhidi ya MO Bejaia kutokana na kadi mbili za njano.
Kuelekea mechi hiyo Yanga inakwenda kukamilisha ratiba kutokana na ushindi ambao Medeama ilipata jana dhidi ya TP Mazembe ambapo kwa matokeo hayo Yanga haitaweza kufikia idadi ya Pointi 8 ilizokusanya Medeama.
Pia Yanga itashuka dimbani wiki hii dhidi ya Azam katika mechi ya ngao ya hisani ikiwa ni sehemu ya ufunguzi wa ligi kuu inayoanza Agosti 20 wikiendi hii.

Comments
Post a Comment