Manchester united inazidi kuwasha moto EPL baada ya kuichapa Southampton bao 2-0 zilizofungwa na Ibrahimovic.
Ibrahimovic maarufu kama Cadabra alifunga bao la kwanza kipindi cha kwanza na bao la pili katika dakika 45 za pili kwa mkwaju wa penati baada ya Luke Shaw kufanyiwa madhambi na Clasie ndani ya sita.
Hii ni mechi ya pili mfululizo Zlatan anachungulia nyavu baada ya kufanya hivyo dhidi Bournemouth wiki iliyopita na sasa anakamilisha idadi ya goli 3.
Mbali na magoli hayo yaliyofungwa na Ibrahimovic pia Mfaransa Paul alifanya vizuri katika eneo la katikati na kuwafanya Oriol Romeu pamoja Steven Davies kupata shida eneo la kiungo.

Comments
Post a Comment