Mshambuliaji wa Manchester united Zlatan Ibrahimovic amesema kuwa yeye kama Simba mwenye njaa ndani ya uwanja.
Ibrahimovic alisema kuwa si kwamba anaweza kila kitu kwenye maisha lakini anatambua jukumu lake ni kufunga uwanjani.
"Mimi si zaidi ya kila kitu lakini ni kama simba mwenye njaa kali niwapo uwanjani, nina kiu ya kufunga." Alisema Ibrahimovic
Mbali na hayo Ibra Cadabra aliongeza kuwa yapo mambo ya msingi kwenye maisha mbali na watu wafikiriavyo, ni mchezaji anayejari na kuheshimu familia yake.
"Naheshimu familia yangu mimi ni mtu mwenye majukumu nadhani familia ni muhimu kwangu, na nina mipaka ya kufanya mambo yangu kuilinda familia." Aliongeza Ibrahimovic.

Comments
Post a Comment