4-3-3 inanoga Simba kuliko kuliko 4-4-2


Katika timu ya Simba kumeanza kuwepo na maelewano baina ya Laudit Mavugo pamoja na Ibrahim Ajib, na taratibu wanamkaribisha Shiza kichuya.

Lakini sijui ni kwanini mwalimu Joseph Omog ambaye ni kocha wa Simba anatumia mfumo 4-4-2 ikiwa washambuliaji wana kasi zaidi uwanjani.

Laudit Mavugo anaonekana kuwa mbunifu wa hali ya juu kwenye kutafuta nafasi za kufunga wakati fulani anaonekana kushoto akitokea na mpira, wakati mwingine kulia au katika wakati huu Shiza Kichuya au Ibrahim Ajib wakiziba ile mianya.

Kwa upande wangu naona kuna matokeo chanya zaidi endapo Joseph Omog atatumia mfumo wa 4-3-3 kuliko 4-2-2 wa sasa, nadhani washambuliaji wa sasa wanaocheza Simba katika safu ya ushambuliaji ni wajanja, wanakasi na wenye vipaji vya hali ya juu nadhani mwalimu ana nafasi ya kuangalia upya mfumo wake.

Si mbaya pia kama timu itaanza na Jonas Mkude, Mzamiru Yasin na Mwinyi Kazimoto/Said Ndemla ambao ni viungo watatu na safu ya ushambuliaji ikawahusisha Mavugo, Ajib na Kichuya.

Mwinyi kazimoto anauwezo mkubwa wa kuendesha mpira na kuongoza mashambulizi kuwatafuta Mavugo, Ajib pamoja na Kichuya, wakati huo Jonas mkunde pamoja na Mzamiru wakisimama upande wa chini kuhakiki mipira kushoto na kulia.

Nadhani Simba inaweza kuwa na magoli mengi katika mechi zao na kupata ushindi mnono kila mara, sawa na vile alivyomaliza kocha wa Yanga Hans Pluijm.

Haya ni maoni yangu kulingana na muonekano mzima wa kikosi cha Simba na aina ya wachezaji walionao sasa, unaweza pia kuchangia maoni yako mbalimbali kulingana na jinsi unavyoiona timu ya Simba kwa upande wako.

Comments