African Lyon inavyoteza mechi nyumbani, itakuwaje mikoani?


Wiki iliyopita nilizumgumzia kuhusu mtazamo mzima wa kikosi cha timu ya Majimaji ya Songea ambayo haijashinda mechi yoyote hadi sasa, nadhani ipo haja ya kuiangalia African Lyon ambayo inaongozwa chini Mreno Fernando Tavares.

Kwa upande wangu naitazama African Lyon inashindwa kunishawishi nadhani kuna haja ya mwalimu Tavares kubadilisha mambo kwenye kikosi chake ambacho kimepata ushindi dhidi ya mbao FC pekee.

Jana timu hiyo imepoteza mechi kwa Kagera Sugar kwa makosa yanayofanana yale waliyofungwa kwenye mechi na Yanga na kuwafanya Danny Mrwanda pamoja na Seleman Mangoma kufunga hesabu ya bao 2-0 Taifa.

Kuna ubovu katika eneo la ulinzi kwenye timu ambayo mwalimu Tavares anatumia zaidi mabeki 3 nyuma na viungo wengi, kwa ujumla mwalimu Tavares ameshindwa kuisukuma African Lyon kuanzia kati kuelekea mbele.

Mwalimu Tavares amesahau kuwakumbukusha na kurekebisha makosa yao pale kwenye beki yake, nadhani ilikuwa rahis kwao kupata sare na Azam kulingana na aina ya mifumo wanayotumia inafanana.

Ikumbukwe African Lyon haijatoka hadi sasa kucheza mechi yoyote nje ya Dar es Salaam, nadhani huo ni mtihani namba mbili kwa mwalimu Tavares ambaye anatakiwa kuwa na mipango B kule kwenye viwanja wa mikoani ambako ufundi ni mdogo.

Pointi yangu ieleweke kuwa kocha Tavares ana mipango mema na Lyon lakini nakuwa kwenye mshangazo kwa kuwa aina pekee ya mpira ambao upo kwenye mipango ya mwalimu huyo unafana katika viwanja vizuri kama taifa na Chamanzi lakini ameshindwa kupata matokeo licha ya kucheza mechi zote kwenye kiwanja bora.

Itakuwaje endapo Lyon wakatua kambarage au Sokoine, Manungu au CCM kirumba wakiendelea hivi walivyo watapoteza mechi zote za mikoani ndiyo maana nimevutiwa kukushawishi na wewe utambue itakuwaje timu hiyo itakapoanza kucheza mikoani, wamejipanga vipi kwa mechi hizo.

Kama Lyon wangekuwa wanautendea haki uwanja wa taifa wala sina shida nao lakini navutiwa kushirikiana nao kwa maandishi kuwa wana hatari kubwa ya kupoteza mechi za mikoani kama wanashindwa kufanya vizuri kwenye mechi za nyumbani.

Kwa kiasi fulani wantakiwa kujifunza kupitia Ndanda wakiwa Nangwanda, Mtibwa Manungu au Prisons pale Sokoine jinsi wanavyokuwa wagumu kupoteza pointi 3 hata kwa timu kubwa za Simba, Yanga na Azam.

Wanatakiwa kuinua macho na kuangalia suala hili kwa umakini vinginevyo kuna hatari ya kubwa kuwepo kwenye nafasi hatarishi kwenye msimamo wa ligi kuu huko mbele.

Comments