African Lyon waikalisha mbao FC 3-1


Baada ya kufungwa goli 3 na Yanga timu ya African leo ikiwa kwenye uwanja wa taifa imelipa kisasi baada ya kuifunga Mbao FC mabao 3-1 katika mechi ya ligi kuu.

Mbao ndiyo walioanza kupata bao kupitia Frank Msiba aliyefunga dakika ya 15 hata hivyo African Lyon ilichomoa bao hilo kupitia Hood  Mayanja aliyefunga kwa mpira wa adhabu nje kidogo ya 18 dakika moja kabla ya kuelekea mapumziko.

Kipindi cha pili African Lyon walirudi kwa kasi na kuongeza bao la pili lililowekwa nyavuni na Hood Mayanja aliyefunga kwa mkwaju wa penati dakika ya 58 na baadae Titto Okello alishindilia bao la tatu dakika ya 68.

Mbao FC imeruhusu mabao 7 ndani ya mechi 2, wiki iliyopita timu hiyo ilipokea kichapo cha mabao 4-1 ilipokutana na Mbeya city.

Comments