Timu ya Azam inajipanga kuendelea na mpango wake wa kusaka vipaji vya soka kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 (U17) ambapo zoezi litafanyika Zanzibar Octoba 6 mwaka huu.
Azam walikamlisha zoezi hilo kwenye mkoa wa Dar es Salaam katika wilaya ya Kigamboni, kinondoni, Ilala na Temeke na kama walivyoahidi wameanza kuhamishia zoezi hilo kwenye mikoa mingine.
Azam ilivuna jumla ya vijana 15 katika mkoa wa Dar es Salaam na sasa inaendelea na mpango wa kukusanya vipaji katika mikoa waliyoipanga ambapo Novemba mwaka huu vijana hao wataingia kwenye mashindano ya mikoa.

Comments
Post a Comment