Timu ya Azam imefanikiwa kuvuna vipaji kumi tano vya soka kwa vijana walio chini ya umri wa miaka 17 na sasa imefunga rasmi zoezi hilo kwa mkoa wa Dar es Salaam.
Azam ilipita katika wilaya zote za mkoa wa Dar es Salaam ikianzia Kigamboni na Temeke pia katika wilaya ya Ilala na Kinondoni ambapo ndipo walipohitimisha zoezi hilo.
Azam ipo kwenye mkakati wa kuandaa timu bora ya vijana wenye umri chini miaka 17 kutokana na kuendelea kwa michakato ya kuanzishwa kwa ligi ya vijana hao na Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania.
Zoezi hilo sasa litahamia katika mikoa mingine ikiwemo Kigoma, Tanga, Arusha na Zanzibar kama ilivyoorodheshwa hapo awali na Uongozi wa Azam.

Comments
Post a Comment