Azam yaingia kambini kujiandaa na Ndanda


Baada ya kipigo cha bao moja kutoka kwa Simba timu ya Azam jana imezama rasmi kambini kujiandaa na mechi ya Ligi kuu dhidi ya Ndanda FC.

Azam ambayo inanolewa na Mhispania Zeben Hernandez ina kibarua kizito cha kupigania pointi 3 katika uwanja wa Mangwanda sijaona mkoani Mtwara.

Msemaji wa timu ya Azam Jaffar Idd alisema kuwa kila mechi inahitaji maandalizi ikiwemo na ya Ndanda kwa kuwa ni timu nzuri ambayo ilitoka na ushindi kwenye mechi ya mwisho.

"Ipo haja ya kujiandaa, tumepoteza kwa Simba lakini tunaingia kambini kujiandaa na Ndanda FC." Alisema Idd

"Maandalizi yanahitajika kwa kila mechi na si kwa ajili ya timu kubwa pekee, mechi ya mwisho Ndanda wametoka na ushindani nadhani wapo kiushandani pia ni muhimu kwetu kujiandaa." Aliongeza msemaji huyo.

Comments