Azam imekutana na vipigo mfululizo kutoka kwa Simba na Ndanda FC ya Mtwara katika mechi mbili za mwisho na kupoteza pointi 6 hali ambayo imemfanya kocha huyo kuiweka tayari timu hiyo kupata ushindi.
Zeben alisema kuwa jumamosi kuna mechi ya watani wa jadi kati ya Simba na Yanga hivyo ni lazima watumie nafasi kusogea mbele ili kurejea juu ya msimamo wa ligi kuu.
"Nadhani ipo haja ya kushinda mechi ijayo, ni vizuri mmoja wa wapinzani wetu ambaye ni Yanga amepoteza mechi tukiwa tumepoteza pia, nadhani mechi ya Simba na Yanga inaweza kuwa na faida kwetu." Alisema kocha huyo.
Simba na Yanga zitashuka dimbani siku ya jumamosi katika mchezo wa ligi ambapo siku ya Jumapili Azam wataikaribisha Ruvu Shooting katika uwanja wa Azam Complex.

Comments
Post a Comment