Baada ya kipigo Mourinho awanyima mapumziko wachezaji


Kocha wa Manchester united Jose Mourinho amewataka wachezaji wa timu hiyo kurejea mazoezini baada ya kufungwa bao 3-1 na Watford.

Kocha huyo ameamua kuitumia siku ya leo kwa ajili ya mazoezi baada ya kipigo hicho ili kuiweka sawa timu ambayo imepoteza mechi 3 mfululizo hadi sasa.

Mourinho alifungwa 2-1 na Manchester city, akapoteza mechi na Feyernood baada ya kufungwa bao 1-0 kwenye Europa ligi ukifuatiwa na mchezo wa jana dhidi ya Watford.

Comments