Bale akamua mbaya, Wales ikishinda 4-0


Mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale amezidi kuing'arisha Wales baada ya kutupia goli mbili katika ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Moldova.

Magoli ya wales yalifungwa na Danny Vokes dakika ya 38, Joe Allen dakika ya 44, na Gareth Bale ambaye alimaliza kazi hiyo baada ya kufunga dakika ya 50 na 90.

Ushindi huo unazidi kuingoza Wales taratibu kuendelea kufanya vizuri kwenye mechi zingine za makundi katika mchakato wa kupata tiketi ya kushiriki fainali za kombe la dunia zitakazofanyika nchini Urusi mwaka 2018.

Comments