Timu ya Barcelona jana katika mechi ya mechi ya ufunguzi wa ligi ya mabingwa barani Ulaya imeibuka na ushindi wa 7-0 dhidi ya Celtic katika uwanja wa Camp Nou.
Katika mechi hiyo mshambuliaji nyota wa timu hiyo Lionel Messi aliondoka na mpira baada ya kufunga 'Hat trick' ambapo alifunga idadi hiyo ya magoli 3 kwenye dakika ya 3, 27 na 60.
Mbali na Messi pia mshambuliaji Luis Suarez alifunga bao mbili dakika ya 75 na 88, Neymar alifunga goli moja dakika ya 50 na kiungo Adres Iniesta ambaye alifunga kwenye dakika 59 ya mchezo.

Comments
Post a Comment