Chirwa akilijua goli, Yanga itakuwa balaa VPL


Ingawa kwa sasa wengi hawaelewi ni kwanini kocha wa Yanga Hans Pluijm anamtumia sana mshambuliaji Obrey Chirwa kuliko Amis Tambwe nadhani taratibu wataelewa.

Mategemeo yangu yalikuwa huenda Yanga ikasajili kiungo bora mkabaji kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi, kulingana mechi za kimataifa walizocheza sehemu ya kiungo mkabaji imeonekana kuwa tatizo kwenye timu ya Yanga.

Makocha wengi hupenda kujihami sana, simaanishi hali ya kukaba au kupaki basi bali ni namna ya kupanga timu kulingana na aina ya wachezaji alionao. Ndivyo ilivyo kwa Hans Pluijm ambaye anajihami kwa silaha zake kali za mbele.

Hans anajua kuna udhaifu kwenye eneo la kiungo, ingawa Kamusoko ni kiungo mzuri lakini huwezi kulinganisha uwezo wake wa kukaba na kiungo kama Jonas Mkude. Hivyo ni kiungo mzuri kwenye  uchezeshaji wa timu wa timu hivyo ni wazi Hans amehamishia silaha zake eneo la wapinzani.

Kumtumia Obrey Chirwa, Simon Msuva, Deus Kaseke na Donald Ngoma kunaonesha ni jinsi gani kocha Pluijm hataki kuiachia pumzi timu pinzani, hataki kuwapa uhuru walinzi wa timu pinzani, Kwa mtindo huo ni wazi Pluijm anajihami na kulinda eneo lake la kiungo.

Wanne hao ambao kwa pamoja wanatengeneza safu ya ushambuliaji Yanga wana kasi na umakini wa hali ya juu hivyo huweka ugumu kidogo kwa mabeki wa timu pinzani kusambulia muda mwingi kwenye lango lao.

Ingawa wengi wanaona Tambwe ana uwezo mkubwa wa kufunga lakini kuna vitu vingi anakosa ukilinganisha na Chirwa, Ingawa kwa upande wangu namuona si mfungaji wa mabao kama tambwe ila kasi na uwezo wa kucheza mpira kuliko Hamis Tambwe vinanifanya kumpa nafasi Chirwa.

Ingawa kuna kitu kidogo Chirwa anakosa anapunguza baadhi ya mawazo ya mashabiki na wapenzi wa soka kuwa ni bora kuliko Tambwe kwa baadhi ya mashabiki lakini imani mchezaji huyo kutoka Zambia ana kipaji cha hali ya juu kwenye soka.

Kama Chirwa anatongeza umakini Golini na kutumia vizuri nafasi za kufunga basi Yanga inaweza kuwa moto wa kuotelea mbali katika safu ya ushambuliaji, inaweza kuwa tishio kubwa kwa walinzi wa timu za ligi kuu Tanzania bara.

Kilichobaki ni Chirwa kuwa mtulivu na kufunga mabao mengi, asichezee nafasi za wazi kama alivyokosa katika mechi dhidi ya Ndanda nadhani haya niliyoandika yatakumbukwa na wapenzi wa soka pamoja na mashabiki wa Yanga.

Comments