Timu ya Manchester city inazidi kuonesha ubora wake EPL baada ya kupata ushindi wa tano mfululizo kwenye ligi hiyo.
Man city imeshinda bao 4-0 katika uwanja wa Etihad, katika mechi hiyo De Bruyne alifunga bao la kwanza, Kelechi Ihenacho alifunga bao la pili, Sterling alifunga bao la 3 na lile la mwisho liliwekwa nyavuni na Ilkay Gundon.
Ushindi huu ni wa nane mfululizo kwa Manchester city ambayo haijapoteza mechi yoyote hadi sasa, ikiwa imeshinda mechi 3 kwenye ligi ya mabingwa Ulaya na mechi 5 kwenye ligi ya EPL.

Comments
Post a Comment