Conte achezea 3-0 Emirates


Kocha wa Chelsea Antonio Conte ameendelea kuwa kwenye wakati mgumu England baada ya kupokea kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Arsenal.

Conte amepoteza jumla ya pointi 8 katika mechi tatu za mwisho ikiwemo ile sare aliyoipata dhidi ya Swansea, kipigo kutoka kwa Liverpool wiki iliyopita na Arsenal jana.

Alexis Sanchez, Theo Walcott na Mesut Ozil waliendelea kuifanya siku ya siku ya Conte kuwa gumu baada ya kukamilisha idadi ya mabao mabao matatu yaliyowekwa nyavuni kipindi cha kwanza katika dakika ya 11, 16 na 40.

Kwa upande wa mechi zingine Man utd ilipata ushindi wa bao 4-1 dhidi ya Leicester ambapo nyota mpya wa timu hiyo Paul Pobga alifunga kwa mara ya kwanza, pia Liverpool ilipata ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Hull city.

Comments