Mshambuliaji wa Manchester city Kevin De Bruyne amesema kuwa ana mabadiliko makubwa chini ya kocha wa sasa wa timu hiyo Pep Gurdiola,
Wakati huu Manchester city ikijandaa na mechi dhidi ya Manchester united, De Bruyne alisema kuwa anavutiwa na mtindo wa sasa wa soka ambalo kocha huyo anafundisha na kuridhishwa na matokeo mazuri wanayopata uwanjani.
De bruyne aliongeza kuwa majukumu aliyonayo kwa sasa kwenye timu si kama yale ya awali kwani kuna mabadiliko makubwa ilinganishwa na wakati ule wa Manuel Pellegrini.
"Majukumu yangu ni tofauti na hapo mwanzo, kwa sasa sikabi sana kocha ameniambia nitengeneze zaidi nafasi za magori, nafurahi endapo wenzangu watafunga kupitia pasi zangu." Alisema De Bruyne.
Manchester city itashuka dimbani kesho katika mechi ya ligi kuu dhidi ya Manchester united katika uwanja wa Old Trafford bila mshambuliaji Sergio Aguero ambaye amefungiwa mechi tatu kutokana na kumchezea vibaya beki wa West Ham Winston Ried.

Comments
Post a Comment