Timu ya England jana ikiwa ugenini ilitoka kifua mbele na pointi 3 baada ya kuifunga Slovakia bao 1-0.
England chini ya kocha mpya Sam Allardyce ilipata bao hilo kupitia Adam Lallana aliyefunga dakika ya 90 zikiwa zimesalia sekunde chache kabla ya kumalizika kwa mechi hiyo.
England imeanza vizuri kwenye hatua ya makundi ikiwa ni mwendelezo mzuri wa kuwania tiketi ya kushiriki fainali za kombe la dunia zitakaofanyika Urusi mwaka 2018.

Comments
Post a Comment