FIFA yasambaza waraka mpya kwa wanachama wake


Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa miguu (FIFA) limesambaza waraka mpya kwa wanachama wake, likiwemo Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ukiwataka mameneja wote wa usajili wa wach(ezaji kwa kwa mfumo wa mtandao (TMS-Transfer Matching System Managers) kujiunga na mawasiliano mapya ili kupata taarifa mbali mbali za usajili na uhamisho wa wachezaji.

Mfumo huo ambao unafahamika kwa jina la GPX yaan Global Players Exchange una malengo ya kurahisisha kufanya usajili kwa mchezaji mmoja kwenda timu nyingine ikiwa ni pamoja na kupata msaada wa taarifa kamili za msajiliwa kwa mameneja hao nchi nzima, kwa timu na mashirikisho mbali mbali duniani.

GPX unalingana na mitandao ya jamii unaoweza kuunganishwa kama WhatsApp unaowezesha mawasiliano na ya karibu na hivyo Shirikisho la kimataifa limeagiza kuwa ni lazima mameneja wa TMS, kila klabu na mashrikisho kujiunga na mtandao huo ambao unafanya kazi ulimwengu mzima.

Mamneja wa usajili wa ligi kuu ya Vodacom, ligi daraja la kwanza ya Star Times (SFDL) na Ligi ya Daraja a pili (SDL) watakaoukuwa tayari wanatakiwa kuwasiliana na meneja usajili wa shirikisho la Soka Tanzania (TFF ) ili kupata maelezo ya kina ya namna ya kujiunga na mtandao wa GPX.

Comments