Pep Gurdiola ameendeleza ubabe kwa Jose Mourinho leo kwa mara ya kwanza kwenye ligi ya EPL ameibuka na ushindi wa bao 2-1.
Magoli ya Manchester city yalifungwa na Kevin De Bruyne aliyefunga dakika ya 45, bao la pili lilifungwa dakika ya 32 Kelechi Ihenacho huku lile la Manchester united likifungwa na Zlatan Ibrahimovic dakika ya 42.
Manchester city ilitawala mpira kwa dakika zote 90, Ingawa Manchester utd iliamka kipindi cha pili ndani ya Dakika 10 za mwanzo lakini mabadilisho yalifanywa na Pep yaliendelea kuiweka manchester utd kwenye wakati mgumu.
Matokeo hayo yanaifanya city kuongoza kwenye msimamo wa ligi kuu ya England kwa pointi 12 ikifuatiwa na Chelsea yenye pointi 9.

Comments
Post a Comment