Baada ya kupata matokeo mabovu katika mechi zote ilizocheza ligi kuu Hatimaye Majimaji imemrejesha aliyekuwa kocha wao msimu uliopita Kalimangonga 'Kally' Ongala kuinoa timu hiyo.
Majimaji imeanza kupoteza mwelekeo baada ya kukubali kipigo katika mechi zote 6 ilizocheza na kupelekea uongozi wa timu hiyo kufanya maamuzi ya haraka kumrejesha Kally.
Kally ambaye ni mtoto ni wa mwanamuziki nguli Remmy Ongala ambaye kwa sasa ni Marehemu aliiongoza Majimaji msimu uliopita na kuikoa kwenye nafasi hatarishi ya kushuka daraja.
Majimaji imempa kocha huyo mkataba wa mwaka mmoja ili kurejesha matumaini kwa wana Lizombe hao wa Songea.

Comments
Post a Comment