Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limemteua Sebastian Nkoma kuwa kocha mkuu wa timu ya soka ya wanawake 'Kilimanjaro Queens' kwa mara ya kwanza inakwenda kushiriki mashindano ya kuwani kombe la Afrika Mashariki na kati inayofanyika nchini Uganda Septemba 11 mwaka huu.
Uteuzi wa kocha huyo umeambatana na sambamba na wasaidizi wake ambao ni Hilda Masanche na Edna Lema wakati meneja wa timu hiyo ni Furaha Francis huku mtunza vifaa akiwa Esther Chabruma maarufu kama Lunyamila.
Kilimanjaro Stars itaingia mazoezini Septemba mosi 2016 ambapo wachezaji wa timu hiyo wanatakiwa kuwasili mazoezini katika uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam na kurudi nyumbani siku ya jumapili na siku ya jumatatu timu hiyo itafunga safari kuelekea nchini Uganda.
kulingana na CECAFA michuano hiyo itafanyika jijini Jinja na Tanzania ambayo kwa sasa inaongoza kwenye viwango Afrika ya Mashariki imepangwa kundi B ikiwa pamoja na timu ya Ethiopia na Rwanda.
Kwa upande wa kundi A kuna timu ya Kenya, Burundi, Zanzibar pamoja na wenyeji Uganda, katika msahindano hayo Tanzania itafungua michezo kwa kucheza Rwanda Septemba 12 mwaka huu, PIA itacheza na Ethipia Septemba 16.

Comments
Post a Comment