Hivi ndivyo Manchester city ilivyokabwa koo na Celtic zikizitoka 3-3 jana.

Kocha wa Manchester city Pep Gurdiola ameshindwa kutamba mbele ya Brendan Rodgers ambaye ndiye kocha wa sasa wa Celtic baada ya kutoka sare ya kufungana mabao 3-3.

Dembele akishangilia moja ya bao alilofunga

Bao za Celtic zilifungwa na mshambuliaji mahili Dembele aliyefunga mara 2 na lingine alijfunga Raheem Sterling huku kwa upande wa city magoli yao yakizamishwa wavuni na Raheem Sterling, Fernandinho na Nolito.

Nolito akishangilia baada ya kuchomoa bao la 3

Kwa upande wa matokeo ya kundi hilo Barcelona ilitoka kifua mbele na pointi 3 baada ya kuifunga Borrusia Moenchenglabacch bao 2-1 nchini Ujermani.

Comments