Licha ya Taifa Stars kupoteza mechi ya jana dhidi ya Nigeria lakini kazi iliyooneshwa na golikipa wa Azam Aishi Manula iliibeba taifa stars na kuwashangaza nyota wanaocheza katika ligi mbali mbali barani Ulaya.
Manula aliwabania nyota wakali wanaong'ara Ulaya Akiwemo Victor Moses (Chelsea), Ahmed Mussa (Leicester cit) na Kelechi Ihenacho (Man city) ambaye ndiye mfungaji wa bao pekee la ushindi wa timu ya Nigeria.
Juhudi kubwa iliyofanywa na Manula ilimfanya aibuke na kuwa nyota wa mchezo (Man of the Match) huo na kuweka kumbukumbu yake binafsi katika nchi hiyo.

Comments
Post a Comment