Mshambuliaji kinda wa timu ya Manchester city Kelechi Ihenacho ndiye aliyewafunga Taifa Stars bao pekee la ushindi na kuinyanyua Nigeria kidedea kwenye mchezo wa jana.
Ihenacho ana miaka 19 tu, alikulia katika kituo cha kukuza vipaji vya soka kinachoitwa Taye Academy kinachopatikana huko Owerri nchini Nigeria ambako Manchester city ilimwona na kumsajili nyota huyo.
Kasi na umakini wake uwanjani vimefanikisha kumshawishi kocha wa sasa wa Manchester city Pep Gurdiola kumtumia mchezaji kama mbadala wa Sergio Aguero na hii imemfanya mshambuliaji wa Ivory Coast Wilfrey Bony kutimka Stoke city kwa mkopo.
Licha ya kiwango bora kilichooneshwa na Aishi Manura jana, lakini dogo huyo ndiye aliyeweza kuichana nyavu ya Taifa Stars na kuifanya Stars kulala kwa goli 1-0.

Comments
Post a Comment