Aleksander Ceferin kutoka Slovenia ndiye mrithi wa Michael Platin baada ya kuchanguliwa kuwa raisi mpya wa soka barani Ulaya (UEFA).
Ceferin 49, anasimama kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Michael Platin ambaye mwaka mmoja uliopita alijiuzulu kwenye nafasi hiyo baada ya kufungiwa kujihusisha na shughuli za soka kwa muda wa miaka 8.
Raia huyo wa Slovenia anakuwa raisi wa 7 kuiongoza UEFA ndani ya miaka 62 tangu kuanzishwa kwa umoja huo, na sasa atachukua kipindi chote kilichochwa na Platin hadi mwaka 2019.

Comments
Post a Comment