Chama cha soka cha England (FA) kimemtua mwamuzi maarufu kwenye ligi hiyo Mark Clattenburg kuamua mechi ya leo kati ya Manchester united na Manchester city.
Clatternburg ambaye amezidi kujizolea umaarufu kwenye ulimwengu wa soka, ndiye mwamuzi aliyechezesha fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya pamoja na fainali ya UEFA Euro nchini Ufaransa.
Manchester united inakutana na Manchester city ambao wote kwa pamoja hakuna aliyepoteza wala kutoa sare katika mechi tatu walizocheza wakiwa na idadi sawa ya pointi 9 kwenye msimamo wa ligi kuu.

Comments
Post a Comment