Jinamizi la Simba lazidi kuitafuna Azam Mtwara


Timu ya Azam jana katika uwanja wa Nangwanda sijaona imepoteza mechi ya pili baada ya kupokea kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Ndanda.

Azam ilipoteza mechi iliyopita katika uwanja wa uhuru baada ya kufungwa bao 1-0 na Simba, hivyo timu hiyo imepoteza pointi 6 kwenye mechi 2.

Kwa matokeo hayo simba inaiacha Azam kwa idadi ya pointi  6 na endapo Yanga itashinda mechi ya leo basi itasogea hadi nafasi ya pili kwenye msimamo.

Ndanda imeanza kujiwekea rekodi nzuri kwa Azam baada ya kukataa kufungwa katika michezo miwili ya mwisho iliyokutana na Azam ikiwemo sare ya mabao 2-2 kwenye mechi ya mwisho pale Chamanzi.

Comments