John Bocco ndiye mchezaji bora mwezi Agosti.


Mshambuliaji na nahodha wa timu ya Azam John Bocco ndiye mchezaji bora wa mwezi Agosti wa ligi kuu Vodacom baada ya kushinda tuzo hiyo.

John Bocco amefunga mabao matatu hadi sasa likiwemo lile la kuisawazishia timu yake katika mechi ya kwanza dhidi ya African Lyon katika mechi ya kwanza.

Pia Bocco alifunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Majimaji ya Songea katika uwanja wa Azam pale Chamanzi Complex.


Comments