Kaseja apata shavu timu ya taifa ya soka la ufukweni


Kocha mkuu wa timu ya taifa ya soka la ufukweni John Mwansasu amemwita golikipa wa zamani wa timu ya Simba Juma Kaseja kuongeza nguvu kwenye kikosi chake kitakachokwenda Abidjan nchini Ivory Coast katika mchezo wa marudiano  dhidi ya timu hiyo.

Mwansasu amesema kuwa Kaseja ni msaada mkubwa kutokana na mbinu nyingi alizonazo kipa huyo ambaye kwa sasa anaitumikia timu ya Mbeya city akimtaka kusaidiana na goli kipa wa timu hiyo Ahamed Rajab.

Kwa upande wa Kaseja amefurahia na kuitikia wito huo na wakati wowote kuanzia sasa anatarajiwa kujiunga na kamb hiyo iliyopo kwenye Hosteli za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), uwanja wa kumbukumbu ya Karume , Ilala jijini Dar es Salaam.

Mbali na Kaseja nyoata wengine wanaounda kikosi hicho ni Talib Ame, Ahamada Ahamad, Mohammed Makame, Ahmed Rajabu (Golikipa), Khamis Said, Yacob Mohamed Ally Raby, Mwalimu Akida, Khalifa Mgaya, Rolland Revocatus, Juma Sultan, Rajab Ghana, Samwel Salonge, Kashiru  Salum, Juma Juma na Kevin Baraka.

Timu hiyo inatarajiwa kuondoka nchini kuelekea Abidjan Septemba 14 mwaka huu kukamilisha ratiba ya mwisho ili kujua nani atafanikiwa kufuzu na kusonga mbele kwenye michuano hiyo. 

Comments