Timu ya taifa ya wanawake Tanzania bara jana imetwaa kombe la ukanda la ukanda Afrika Mashariki na kati (CECAFA) maarufu kama Challenji baada ya kuifunga Kenya Mabao 2-1.
Kwa upande wa wanawake Queens wanaweka rekodi ya kutwaa kombe hilo kwa ukanda wa Afrika Mashariki na kati ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika kwa mashindano kwa upande wa wanawake.
Safari ya ushindi kwa kilimanjaro Queens ilianzia mkoani Kagera ambako waliweka kambi ndogo na kujipima nguvu dhidi ya timu ya taifa ya Burundi na kuichapa bao 3-0 katika uwanja wa kaitaba.
Queens pia ilianza vizuri katika mechi za makundi baada ya kuifunga Rwanda mabao 3-2, ikatoa sare na Ethiopia na kufanikiwa kutinga nusu fainali ambapo iliweza kumwondoa mwenyeji Uganda hadi kufikia jana katika fainali ya kombe iliilaza Kenya kwa kipigo cha bao 2-1.
Huu ni mwanzo mzuri kwa Queens ambao wameonesha mwanga kwa taifa na huenda sasa kikosi hicho kikaendelea kufanya vizuri zaidi katika mashindano mengine barani Afrika.

Comments
Post a Comment