Timu ya taifa ya wanawake Tanzania 'Kilimanjaro Queens' imeanza vizuri kwenye mechi za kujipima nguvu baada ya kuifunga Burundi bao 3-0 kwenye mechi ya kirafiki iliyochezwa Kaitaba Kagera.
Magoli ya Kilimanjaro Queens yalifungwa na Asha Rashidi aliyeanza kutikisa nyavu kwenye dakika ya 28, dakika 10 baadae aliyekuwa nyota wa mchezo huo Mwanahamisi Omary aliipatia Queens bao la bao la pili na bao la tatu lilipatikana dakika ya 42 baada ya mchezaji wa burundi kujifunga kutokana na shuti kali lililopigwa na Asha Rashid.
Kipindi cha Pili timu zote zilionekana kutulia zaidi na kucheza kwa umakini wa hali ya juu hali iliyopekelekea kukosekana kwa magoli kwenye kipindi hicho na mpira kumalizika Queens wakitoka kifua mbele kwa ushindi wa mabao 3.

Comments
Post a Comment