Klopp: Mashabiki msiimbe jina langu kabla ya matokeo


Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amewataka mashabiki wa timu hiyo wasiimbe jina lake mpaka timu hiyo itapokuwa na uhakika wa matokeo ya ushindi.

Mashabiki wa Liverpool walifanya hivyo katika ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya Arsenal pia katika mechi ya jana ambayo ambayo walipata ushindi wa mabao 4-1.

Hatua hiyo haijamridhisha Klopp ambaye ameowaomba mashabiki kuimba jina lake iwapo timu hiyo itakuwa imepata matokeo ya uhakika na yanaoonesha dalili ya ushindi kwa Liverpool.

"Tafadhali msiimbe jina langu kabla ya kupata matokeo kamili, nataka kuwa upande mmoja na wachezaji, ingawa sichezi uwanjani lakini najisikia sawa na wao." Alisema Klopp

Katika mechi ya jana Liverpool iliibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Leicester, magoli hayo yalifungwa na Roberto Firmino ambaye alifunga mara mbili, Sadio Mane na Adam Lallana.

Comments