Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema kuwa anaweka mikakati kabambe ya kukabiliana na mshambuliaji tishio wa Chelsea Diego timu hizo zitakapokutana kwenye uwanja wa Stamford Bridge hapo kesho.
Klopp amesema kuwa kucheza uwanjani na mshambuliaji tishio kama Diego Costa hakuhitaji urafiki na kuongeza kuwa mshambuliaji ana nguvu na kuna wakati inakuwa ngumu kumzuia.
"Diego Costa ni mpambanaji hasa, haitaji urafiki uwanjani, ana nguvu na ana kipaji cha kutumia mwili wake vizuri ni moja kati ya washambuliaji wazuri duniani, nadhani alionekana hadhuiriki katika mechi ya Swansea." Alisema Klopp
"Kwa sasa mshambuliaji huyo ametengeneza mahusiano mazuri na kocha wake (Antonio Conte), amerejea kwenye ubora. Ni mchezaji tishio" Aliongeza Klopp.
Liverpool na Chelsea zipo kwenye maandalizi ya mwisho ya mchezo wa kesho wa ligi kuu England, Chelsea ikiwa nyumbani itaikaribisha kwenye mechi ya kesho.

Comments
Post a Comment