Klopp: tutatumia mashabiki kuishinda Leicester


Kocha wa Liverpool Juegen Klopp amesema kuwa siri pekee ya kuishinda Leicester city ni kutumia vizuri nguvu ya mashabiki wao katika uwanja wa Anfield kesho.

Kwa mara kwanza Liverpool itakuwa kwenye uwanja wa Anfield tangu kuanza kwa msimu wa ligi baada ya mechi zote tatu za awali kucheza ugenini ikiwemo ile ya Arsenal, Burnley na Tottenham.

Liverpool inajivuna baada ya kuongeza idadi ya majukwaa kwenye uwanja wao ambapo kwa sasa Anfield ina uwezo wa kubeba idadi ya mashabiki wasiopungua 54078 tofauti na ile idadi ya awali ambayo ilikuwa ikibeba jumla ya mashabiki 45362

"Ni furaha sana kwenye timu, idadi ya mashabiki wasipongua 8000 wanaongezeka uwanjani, morali yetu itakuwa juu  nadhani tunaweza kuishinda Leicester kwa nguvu ya mashabiki tuliyonayo." Alisema Klopp.

"Ni timu yetu pekee imecheza mechi tatu mfululizo ugenini, nadhani hii ni nafasi nzuri kwetu tumerejea nyumbani na mashabiki wengi watakuwa nasi." Aliongeza kocha huyo.




Comments