Matarajio ya wengi leo ni hamu ya kujua nani ataibuka mbabe kati ya Simba na Azam ambao mbabe alikosekana msimu uliopita.
Kwa upande wa Azam John boko 'Adebayor' yuko vizuri na ataanza katika mchezo wa leo hivyo safu ya ulinzi ya Simba inatakiwa kuwa makini.
Lakini hii si kwa Simba pekee, Azam pia wanatakiwa kuwa makini katika safu ya ulinzi , uwepo wa Laudit Mavugo katika eneo la mbele itawapa wakati mgumu mabeki wa Azam.
Kwa pamoja Simba na Azam wana safu nzuri ya kiungo, nadhani kutakuwa na mpira mzuri siku ya leo, kutakuwa na soka la kuvutia.
Viungo wa timu zote mbili wana nafasi kubwa ya kuamua matokeo siku ya leo, nadhani viungo watakaotengeneza nafasi nyingi wana nafasi kubwa ya kuamua matokeo ya ushindi.
Azam na Simba wote kwa pamoja wana pointi 10 nadhani kuna nafasi ya mmoja kuondoka na pointi kumi 15 siku ya leo, au mmoja kuzikosa na wakagawana pointi, yote yanawezekana. Mpira ni mchezo wa dakika 90.

Comments
Post a Comment