Kama ilivyo kawaida pale inapokaribia mechi ya watani wa jadi kati ya Simba na Yanga mbwembwe na vioja vya kutosha huendelea kujitokeza mtaani, yakiwemo malumbano pamoja na majigambo ya hapa na pale.
Jana nikiwa maeneo flani ya Dar es Salaam palikuwa na ugomvi mkubwa baina watu wawili ambao ilibaki kidogo wakunjiane ngumi ambapo chanzo kilikuwa ni ushindani wa maneno kuwa ni nani ataondoka na pointi 3 kesho katika uwanja wa taifa.
Kuelekea mechi ya Simba na Yanga tayari kuna vikundi mbalimbali vya kufanya vituko na kebei vimeandaliwa ikiwemo na vikundi vya ngoma kama ilivyo kawaida.
Moja ya vioja vya mashabiki kabla ya mechi
Kwenye matawi mbalimbali mashabiki wa timu zote mbili wanonekana kujipanga vema kwa ajili ya kwenda kupokea burudani ya dakika 90.
Hakika Simba na Yanga haishi vioja huko mitaani kuna mambo mengi nitandelea kukuhabarisha usikae bali na blog hii ambayo inakuleta karibu na michezo.

Comments
Post a Comment