Leicester yaanza na ushindi ligi ya mabingwa, yaichapa Club Brugge bao 3-0


Timu ya Leicester imepoza machungu ya kipigo ilichopata kwa Liverpoool baada ya jana kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Club Brugge.

Kiungo wa Leicester Marc Albrighton alianza kufungua ukurasa wa mabao dakika ya 5 tu ya mchezo baada kutupia wavuni bao la kwanza, na Mahrez alifunga mawili dakika ya 29 na 61.

Ushindi huo umeinyanyua Leicester kuongoza kundi G hii ni baada ya FC Porto kupata matokeo ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Koebenhavn.

Comments