Timu ya Liverpool jana imeondoka na pointi 3 katika uwanja wa Stamford Bridge baada ya kuifunga Chelsea bao 2-1.
Liverpool ilitawala vema mpira kipindi cha kwanza na kuweza kupata mabao mawili ya kuongoza kupitia Dejan Lovren aliyefunga dakika ya 16 na Jordan Henderson aliyefunga dakika 36.
Kipindi cha pili Chelsea walionekana kurejea kwenye hali yao kutokana kuliandama lango la Liverpool kwa muda mwingi na kuweza kupata bao la kufutia machozi kupitia Diego Costa aliyefunga dakika ya 62.
Kwa matokeo hayo yanaifanya Liverpool kulingana pointi na Chelsea ambazo kwa pamoja wana pointi 10 kila mmoja.
Mbali na Mechi hiyo siku ya leo kutakuwa na mechi mbali mbali ligi kuu England ikiwemo mechi kati ya Arsenal na Hull city na Manchester city wataika FC Bournemouth.

Comments
Post a Comment