Liverpool yamkalisha bingwa mtetezi 4-1


Timu ya Liverpool jana ikiwa kwenye uwanja wa Anfield imetoka kifua mbele baada ya kupata ushindi mnono wa mabao 4-1 dhidi ya Leicester city.

Liverpool ambayo kwa mara kwanza ilicheza kwenye uwanja wa nyumbani tangu kuanza kwa msimu mpya wa ligi ilipata magoli ya ushindi kupitia Roberto aliyefunga goli dakika ya 13 na 89, Sadio Mane dakika ya 31 na Adam Lallana dakika ya 56.

kwenye mechi hiyo Liverpool walicheza kwa kasi kubwa uwanjani na kushambulia kwa haraka hali iliyowafanya Leicester city kuruhusu bao nne bila kipingamizi.

Safu ya ushambuliaji ya Liverpool chini ya Sadio Mane, Daniel Sturridge na Roberto Firmino ilivunja ukuta imara ambao unasimamiwa na nahodha wa Leicester Wes Morgan pamoja na Robert Huth..


Comments