Llorente: Conte atabeba ubingwa EPL


Mshambuliaji wa zamani wa Juventus Fernando Llorente ana imani kuwa kocha wa sasa wa Chelsea Antonio Conte ataiongoza timu hiyo kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu huu.

Llorente ambaye leo ataingoza Swansea kuikabili Chelsea kwenye uwanja wa Liberty amesema kuwa Conte ni kocha mwamasishaji, mwenye mbinu nyingi na anayependa kujenga heshima kwa wachezaji wake.

"Nadhani kuna kitu Conte anaongeza ndani yao, nilipokuwa Juve ilikuwa hivyo, Conte hutuhamasisha sana katika vyumba vya kubadilishia nguo hakika itakuwa hivyo hadi mwisho wa msimu kwa timu ya Chelsea." Alisema Llorente.

Pia nyota huyo wa zamani aliyewika na timu ya Athletic Club ya Hispania amemsifia Diego Costa ni moja kati wa washambuliaji bora ambao anawaheshimu kwenye maisha yake.

"Ingawa anapingwa sana na vyombo vya habari vya Hispania lakini Diego Costa ni mchezaji bora, ana nguvu, kasi na anajituma sana akiwa uwanjani, nimekutana nae mara kadhaa, hatujawahi kugombana na pia nina muheshimu sana." Aliongeza Llorente

Comments